Название | Sayari Saba |
---|---|
Автор произведения | Massimo Longo E Maria Grazia Gullo |
Жанр | Зарубежное фэнтези |
Серия | |
Издательство | Зарубежное фэнтези |
Год выпуска | 0 |
isbn | 9788835424239 |
Maria Grazia Gullo - Massimo Longo
SAYARI SABA
Mifupa ya nje na kitu cha Parius
Imetafsiriwa na Kennedy Cheruyot Langat
Hakimiliki © 2019 MG Gullo - M. Longo
Picha ya Jalada na michoro imeundwa na kuhaiririwa na Massimo Longo
Haki zote zimehifadhiwa
YALIYOMO
Sura ya Kwanza Bahari ya Ukimya | |
Sura ya Pili Upanga wa jiwe ulikuwa ukining'inia juu ya vichwa vyao | |
Sura ya Tatu Mikunjo kwenye Ngozi yake ilidhihirika kwenye macho na mdomo wa kiumbe hicho | |
Sura ya nne Afisa fupi wa jeshi | |
Sura ya Tano Usingizi nzuri kama huo | |
Sura ya Sita Alikumbuka jinsi mzazi angemkumbatia mwanawe | |
Sura ya Saba Umbali huu usiokwisha unaniua | |
Sura ya Nane Mshambulizi huyo alipiga Reveli | |
Sura ya Tisa Kulabu kwenye ncha ya bawa inamwumiza | |
Sura ya Kumi Dimbwi la maji safi | |
Sura ya Kumi na Moja Urembo kama huo katikati ya vita vikali | |
Sura ya Kumi na Mbili Aliingia ndani ya chumba bila kutangaza. | |
Sura ya Kumi na Tatu Alianza kumtazama. Mikono yake ilikuwa ikitetemeka | |
Sura ya Kumi na Nne Tuna maji ya kuzima moto? | |
Sura ya Kumi na Tano Kila kitu kilikuwa kinatetemeka karibu na Ruegra | |
Sura ya Kumi na Sita Fataki moja hewani | |
Ukurasa wa Kumi na Saba Wakiwa wameshikilia silaha zao, walikuwa wakipiga kelele kwa furaha |
Sura ya Kwanza
Bahari ya Ukimya
Jenarali Ruegra alikuwa akitazama angani kupitia shimo kubwa kwenye dirisha ndogo kwenye dambra. Ilivutia kuona mfumo mzima wa sayari wa KIC 8462852 na sayari zake saba kwenye obiti. Wakati huo, angeweza kuona tu sayari tano kati ya hizo: Sayari ya Carimea, ambayo ni nyumbani kwake, ilikuwa na anga ya kijivu, ambayo ilimaanisha ilikuwa imepangiwa nafasi ya uongozi; Medusa ilikuwa ya bluu na ya kupendeza, ambayo ilikuwa na sumaku na hatari kama wakaazi wake; Oria, ambayo ilikuwa ndogo na tasa kama mwezi, na pia ilikuwa nyeupe kutokana na akisi ya mwangaza wa Jua letu. Umbali usio mrefu kutoka Oria, kulikuwa na Sayari ya sita ambayo ilikuwa kijani kibichi, na ambayo ilikuwa na ujamii zaidi na ilikuwa imeendelea kiteknolojia miongoni mwa sayari nyingine; na Eumenide, iliyokuwa na anga ya waridi, ambayo ilikuwa ya kuvutia sawa na wakaazi wake wa kutisha.
Yote hayo hivi karibuni yatakuwa mali ya watu wa Aniki na yeye atateuliwa kiongozi mkuu. Alihitajika kuwa mvumilivu na kukamilisha mpango wake: huku akiwa na Ngozi iliyo na sheria mikononi mwake kila kitu na kila mtu atafanya kulingana na mapenzi yake.
Jenerali Ruegra alikuwa akitazama angani kupitia dirisha ndogo kwenye dambra lake na angehisi tamaa ya uongozi ikikua ndani yake. Ilikuwa mwaka wa 7692 tangu kuanzishwa kwa utawala wa Aniki. Ruegra aliamshwa ghafula kutoka kwenye ndoto ya adhama. Chombo chake cha angani kilikuwa kimegonga kitu: walikuwa wanavuka mviringo wa Bonobo. Ingekuwa bora kuelekea kwenye dambra ya kuthibiti chombo. Ingawa kutua kwenye sayari hiyo ilikuwa utaratibu wa kawaida, bado inaweza kuwa na matatizo kadhaa.
Punde tu alipoingia katika dambra ya kuthibiti chombo, alilakiwa kwa heshima na wasaidizi wake.
Utaratibu haukuwa unaenda vizuri kama ilivyopangwa awali: kuna kitu kilikuwa kimegonga meli hiyo ya angani, kama alivyohofia.
"Jenerali, eneo la 8 limeharibiwa. Jiwe limetugonga. " Nahodha akaripoti mara moja.
"Tenga eneo hilo mara moja na uendelee kuliondoa sehemu hiyo."
Nahodha aliamuru mchakato wa uokoaji katika eneo lililotengwa:
"Uokoaji wa haraka katika eneo hilo ...
Ulitenge! Usipoteze wakati wowote! " "
Afisa huyo mara moja alitekeleza amri hiyo. Hakuna aliyethubutu kumfanya Ruegra aone kuwa hatua hiyo itachukua maisha ya wanajeshi wengi bure.
Kuta nyingi zilizokuwa zikitenganisha eneo hilo kutoka kwa sehemu nyingine za meli hiyo ya angani zilifungwa. Wanajeshi wachache tu ndio walioweza kuruka kwa haraka chini ya mlango uliotenganisha eneo hilo na nyingine ili kuepuka kusombwa. Kwa bahati mbaya, walishuhudia wenzao, ambao walikuwa wameishi pamoja hadi dakika chache zilizopita, wakipoteza matumaini walipogonga kuta hizo na kisha wakatoweka.
Utengaji wa eneo lililoharibika ulikamilishwa, na eneo hilo likaachwa.
Vyombo vyote vya angani vya Carimea vilikuwa vya angani na vilikuwa na umbo la mdudu mkubwa wa trilobiti. Vilikuwa vimegawanya kwa vipande vipande ili eneo fulani liondolewe kwa haraka linapoharibika. Kwa njia hii, wafanyikazi wataafikia matokeo mazuri wakati wa vita. Sehemu zote mbili za katikati na mkia, ambazo zilikuwa na umbo la ganda la chaza, zinaweza kuondolewa. Dambra ya kuthibiti chombo hicho, inayoshirikisha sahani kubwa na sura ya nusu mviringo ambayo inakuwa na pembe nyingi katika sehemu nyingine na kuwa ‘mgongo’ wa chombo hicho, haiwezi kuondolewa.
Zilikuwa zimezungukwa na mnyoosho usio na mwisho zilizoundwa na miviringo kubwa ya kijivu ambayo ilikuwa imezunguka sayari ya Bonobo. Miviringo hiyo ilikuwa inajumuisha vifusi vikubwa vilivyosababishwa na kifo cha kimondo ambacho kilikuwa kimesonga karibu na KIC 8462852.
Bonobo, ambayo ni sayari ya pili iliyo mbali kutoka kibete, pia ilijumuisha donge ambalo lilikuwa limekusanya vifusi vingi. Kwa njia hii, ilikuwa imeacha sayari ndogo ya Enas na ilikuwa imeunda mandhari ya kiajabu katika galaksi yote.
Sayari hiyo ilipatikana katikati ya miviringo hiyo. Ilikuwa ina mali nyingi sana na tofauti hivi kwamba ilitumika kama hifadhi ya kifalme ya Aniki ya uwindaji, watumwa na vifaa. Watu wake ambao walikuwa kama binadamu walikuwa wamekwama katika mwanzo wa utawala wao. Watu wa Bonobo walitembea wima, walikuwa na miguu ya yenye viungo vya kushika na miili yao ilikuwa na manyoya.
Walikuwa kubwa kama masokwe lakini hawakuwa werevu na walikaa kama watoto. Wangezaa haraka na walikuwa na nguvu, ambayo ingawafanya wakimilifu.
Bonobo ilikuwa sayari ya pekee ambayo ilitwaliwa na wana-Aniki ambayo ilisalia chini ya utawala wao. Na ni kwa sababu tu sayari hizo mbili zilikuwa zinafanana na zilikuwa zinazunguka KIC 8462852.
Carimea ilikuwa imeweza kutwaa utawala wa sayari nyingine pia, lakini kila mara walikuwa wanapoteza uthibiti kutokana na uasi uliochochewa na muungano wa sayari hizo nne, ambazo lengo lao lilirahisishwa na kuwa karibu kwa mzingo.
Meli ya angani kilitua kwa wakati ufaao. Katika makao makuu, vifaa tayari vilikuwa vimetayarishwa kwa mgao. Ruegra alishuka chini ili kuongea tu na Mastigo, Gavana wa eneo hilo. Jenerali huyo hakumpenda huyo mtu wa Evic hasa, lakini uongozi wake kwa wakaazi ulikuwa na ufanisi. Alikuwa wa kabila maarufu huko Carimea.
Wa-Eviki walikuwa wakubwa, reptilia wa kijani-kijivu ambao wangetembea kwa miguu yake ya nyuma iliyokuwa minene na yenye nguvu. Walikuwa wadogo kidogo kuliko wa-aniki isipokuwa nyuso zao, ambazo